BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Waandishi wetu

AZAM FC leo imeifunga Ndanda FC bao 1-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyochezwa Uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara na kuifanya timu hiyo ifikishe pointi 19 sawa na Yanga ambao wana mabao mengi ya kufunga.

Kwa matokeo hayo Azam itaendelea kushika nafasi ya pili ikifuatiwa na Stand United yenye pointi 15 sawa na Simba ambao wanashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi hiyo. Bao la Azam lilifungwa na kiraka wao, Shomari Kapombe.

Mkoani Mbeya katika Uwanja wa Sokoine, Mbeya City wameifunga African Sports bao 1-0. Bao la City limefungwa na Geofrey Mlawa ikiwa ni dakika ya 12 tangu mchezo huo uanze huku wakionekana kushambulia lango la wapinzani wao mara kwa mara ingawa mashambulizi yao mengi hayakuwa na madhara.

Mlawa alifunga bao hilo kwa kichwa akiunganisha mpira wa kona uliopigwa na Hamad Kibopile huku wachezaji wa Sports wakiwa wamepoteana langoni kwao.

Mwadui wao wameibuka na ushindi wa bao 3-1 dhidi ya Mgambo JKT mchezo uliochezwa Uwanja wa Mwadui Complex mkoani Shinyanga huku JKT Ruvu wao walikuwa wenyeji wa Mtibwa Sugar ambapo wametoka sare tasa.

Post a Comment

 
Top