BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally, Mbeya.

MBEYA City ilifungwa na Simba bao 1-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyochezwa wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya na sasa imeapa 'kufa' na vibonde wenzao African Sports.

City itacheza mechi hiyo Alhamisi katika Uwanja wa Sokoine ambapo tayari African Sports wameishatua jijini Mbeya.Kocha Mkuu wa Mbeya City, Meja Abdul Mingange amesema kuwa ni lazima washinde mechi hiyo kwani matokeo yao ya mechi ya awali ni mabaya na kuifanya City iendelee kuwa katika nafasi mbaya kwenye msimamo wa ligi.

Alisema kuwa kufungwa na Simba kumewafanya wajitume zaidi ili mchezo ujao wapate pointi hizo za muhimu wakiwa nyumbani ingawa ameweka wazi kuwa Citu ya sasa bado inaendelea kujengeka ambapo itachukuwa muda mrefu kukaa sawa.

''Hapa ni kama tunatengeneza timu hivyo tunahitaji kuwa na subira kwa kipindi hiki. Hii timu ni nzuri sana ila haijapata muda wa kukaa pamoja kwa kipindi kirefu.

''Tulifungwa na Simba hivyo hatuwezi kukubali kupoteza na African Sports lazima ushindi upatikane. Vijana wangi wanajituma ingawa nitamkosa Raphael Alfa ambaye ameumia kisigino,'' alisema Mingange.

Mingange alisema kuwa ya sasa ni ngumu na ina upinzani mkubwa na  hivyo kila timu inayoingia uwanjani inajiandaa kwa kila mbinu kihakikisha inapata ushindi.

Post a Comment

 
Top