BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Christian Simba
CHELSEA leo imekubali kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa vijogoo wa Anfield, Liverpool, katika mechi ya Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) iliyopigwa kwenye dimba la Stanford Bridge, maarufu kama ‘Darajani’.


Chelsea ambayo imepata kichapo hicho ikiwa nyumbani walianza kupata bao la kuongoza dakika ya nne tu baada ya mchezo huo kuanza kupitia kwa Ramires na kabla ya kipenga cha kwenda mapumziko kupulizwa , Philippe Coutinho akaisawazishia bao Liverpool dakika ya 45.


Kipindi cha pili Chelsea walionekana kuelemewa katika mchezo huo kutokana na mashambulizi yaliyokuwa yakifanywa na Liverpool yaliyozaa bao la pili lililofungwa na Coutinho na baadaye Benteke akaihakikishia Liverpool pointi tatu kwa kutia nyavuni bao la tatu dakika ya 86.


Baada ya kipigo hicho kibarua cha Kocha Jose Mourinho kinaripotiwa kuwa shakani kutokana na shinikizo kubwa analolipata kutoka kwa wamiliki na mashabiki wa klabu hiyo  wanaotaka aachishwe kazi kutokana na muendelezo wa matokeo mabaya anayoyapata na kikosi chake.

Post a Comment

 
Top