BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Christian Simba
CHELSEA leo Jumamosi wana kibarua kingine cha kuwakaribisha Liverpool kwenye dimba lao la Stamford Bridge ikiwa ni mechi ya Ligi ya Premia.

Vijana wa Jose Mourinho wamekuwa wakipata  matokeo mabaya msimu huu, jambo ambalo linamuweka katika wakati mgumu Meneja huyo na kukabiliwa na shinikizo la kubadili mambo.

Chelsea wameshinda mechi moja pekee kati ya sita walizocheza karibuni zaidi katika mashindano yote.
The Blues wamefungwa mabao 19 Ligi ya Premia,  Norwich wamefungwa mabao 21, Bournemouth na Newcastle wote wakiwa wamefungwa mabao 22 kila mmoja na ndiyo wanaoongoza kwa kufungwa mabao mengi msimu huu.


Mshambuliaji wao Diego Costa huenda akacheza lakini bado kuna shaka kuhusu Pedro ambaye anafuatiliwa kwa karibu baada ya kurejelea mazoezi.

Pia watawakosa Branislav Ivanovic na Thibaut Courtois. Nemanja Matic, aliyepigwa marufuku mechi moja atarejea uwanjani baada ya kutumikia adhabu  hiyo mechi dhidi ya Stoke katika Kombe la Ligi.

Upande wa Liverpool, meneja wao mpya Jurgen Klopp anaweza kumtumia Christian Benteke lakini Daniel Sturridge bado anauguza jeraha pamoja na Kolo Toure.

Akizungumza na wanahabari leo Mourinho amesema, “Matokeo sasa yamekuwa kila kitu (hasa kwenu wanahabari). Ni jambo la kushangaza kwamba miezi michache iliyopita nilishinda mechi nyingi na nikawa bingwa wa Uingereza, watu walikuwa wakisema kuna mambo muhimu zaidi kushinda matokeo,”.

Kwa upande wake, Klopp amesema Chelsea bado ni hatari. “Sina uhakika kwamba ni rahisi kucheza dhidi ya Chelsea leo kuliko mwaka jana. Kwanini iwe hivyo?”

Liverpool walishinda mechi tatu mfululizo Stamford Bridge mwaka 2011 lakini hawajashinda hata mechi moja tangu wakati huo.
Mechi nyingine zitakazochezwa wikiendi hii ni kama ifuatavyo:

 Leo Jumamosi Oktoba 31, 2015
15:45 Chelsea vs Liverpool
18:00 Swansea City vs Arsenal
18:00 West Bromwich Albion vs Leicester City
18:00 Crystal Palace vs Man  United
18:00 Manchester City vs Norwich City
18:00 Newcastle United vs Stoke City
18:00 Watford vs West Ham United

Jumapili Novemba 1, 2015 Jumapili, Nov. 1
16:30 Everton vs Sunderland
19:00 Southampton vs AFC Bournemouth

Post a Comment

 
Top