BOIPLUS SPORTS BLOG

ENGLAND imefuzu kwenda Euro 2016 kwa mtindo wa aina yake baada ya kushinda mechi zake zote 10 katika hatua ya makundi.

Hiyo ni baada ya Lithuania kukubali kichapo cha mabao 3-0 mbele ya England iliyojikusanyia jumla ya pointi 30 na magoli 31 huku ikiwa imeruhusu nyavu zake kutikisika mara tatu tu.

Goli la kwanza la England lilifungwa na kiungo wa Everton Ross Barkley kunako dakika ya 29 kabla ya kipa Giedrius Arlauskis hajajifunga dakika ya 35 katika juhudi zake za kuokoa.

Mshambuliaji wa Arsenal Alex Oxlade-Chamberlain akaihakikishia ushindi England baada ya kufunga bao la tatu dakika ya 62.


Post a Comment

 
Top