BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally, Dar.

MSHAMBULIAJI wa Vipers na timu ya Taifa ya Uganda 'Cranes', Erisa Ssekisambu amesema kuwa ana mkataba wa miaka mitatu na klabu yake ya Vipers lakini yupo tayari kuondoka kama Simba watakuwa tayari kuvunja mkataba huo na klabu yake.

Kumekuwepo na taarifa za Wekundu hao wa Msimbazi kutaka saini ya mshambuliaji huyo aliyeiuwa Taifa Stars kwenye mechi ya kuwania kufuzu michuano ya CHAN lakini yeye amesema kuwa njia pekee ya kumng'oa hapo ni Simba kumalizana kwanza na klabu hiyo.

Erisa alisema kuwa yeye kama mchezaji hawezi kuchagua timu ya kuchezea kwani hiyo ndiyo kazi yake lakini kikubwa anachopenda kizingatiwe ni kufuata taratibu za usajili.

''Simba bado hawajanifuata, kama wana mpango huo mimi sina tatizo ila wao ni kufuata taratibu kwa kumalizana na viongozi wangu kwani nina mkataba wa miaka mitatu.


''Wakimalizana na klabu kwangu itakuwa rahisi nipo kwa ajili ya kucheza mpira na ndiyo kazi yangu lakini siwezi kusema nitacheza Simba au nakuja Simba wakati viongozi wa Simba hakuna taratibu yoyote iliyofanyika wakileta pesa hakuna shida,'' alisema Erisa.

Simba pia imewaweka mawindoni winga Brain Majegwa ambaye suala lake na Azam lipo TFF, Kevin Ndayisenga, Laudit Mavugo ambao ni raia wa Burundi, Farouk Miya wa Vipers na Edmore Charambadare raia wa Zimbabwe huku pia mshambuliaji wao Raphael Kiongera naye akitajwa kurejeshwa kikosini.

Post a Comment

 
Top