BOIPLUS SPORTS BLOG

LIGI Daraja la Kwanza chini (FDL) inatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa michezo 12 kuchezwa katika viwanja mbalimbali kutoka katika makundi yote matatu ya A, B, na C.
Kiungo wa Friends Rangers, Mohamed Banka(kushoto)

Ijumaaa African Lyon watakuwa wenyeji wa Polisi Dodoma katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam, ukiwa ni mchezo wa kundi A.

Jumamosi Kundi A, Mjii Mkuu (CDA) watakua wenyeji wa Kiluvya Uinted katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, KMC wakiwakaribisha Polisi Dar kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.

Kundi B, Kimondo FC watawakaribisha Polisi Morogoro uwanja wa Vwawa – Mbozi, Burkinafaso dhidi ya Kurugenzi uwanja wa Jamhuri Morogoro, Njombe Mji dhidi ya JKT Mlale uwanja Amani Njombe.

Kundi C, Mbao FC dhidi ya Panone FC uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, Rhino Rangers dhidi ya Polisi Mara uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Tabora, Geita Gold Vs Polisi Tabora uwanja wa Nyankumbu Geita na JKT Kanembwa Vs JKT Oljoro uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Ligi hiyo itaendelea siku ya Jumapili kwa michezo miwili kuchezwa, Ashanti United watawakaribisha Friends Rangers uwanja wa Karume jijini Dar es salaam, huku Ruvu Shooting wakiwa wenyeji wa Lipuli FC katika uwanja wa Mabatini Mlandizi mkoani Pwani.

Post a Comment

 
Top