BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Christian Simba.

KOCHA wa Bayern Munich ya Ujerumani, Pep Guardiola amesema kuwa kuelekea mchezo wao wa klabu bingwa Ulaya dhidi ya Arsenal, klabu yake itaingia uwanjani kama wanyonge kwa Arsenal kwakua Arsenal wanahitaji kushinda.

Kauli hiyo ya Guardiola inaonekana kama ni ya kuwapa moyo Arsenal ambao wamepoteza michezo yao yote miwili ya awali dhidi ya Dynamo Zagreb na Olimpiakos Piraeus.


Klabu ya Bayern Munich hadi sasa haijapoteza mchezo wowote katika michezo 12 ya mashindano yote huku wakiwa wametupia mabao 40 na kuruhusu matano pekee. Kikosi cha Arsenal kinahitaji ushindi katika mchezo wa leo ili kufufua matumaini ya kuvuka hatua ya makundi.


Rekodi hii ya Bayern inawaweka katika mazingira mazuri ya kushinda mchezo huo kwani hadi sasa hawajawahi poteza mechi hata moja.Guardiola akiongea na vyombo vya habari amesema kuwa wanahitaji kuwaheshimu sana Arsenal kwani ni miongoni mwa timu kubwa na mahiri barani Ulaya.


Arsenal wanashika mkia katika Group F wakiwa na pointi 0 katika mechi mbili walizocheza.Aidha Arsene Wenger kocha wa Arsenal amesema kuwa haoni ajabu kuelekea katika mchezo huo kwani Arsenal tayari ilikwisha wahi ifunga Bayern Munich huko nyuma katika michuano kama hii.

Post a Comment

 
Top