BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
UONGOZI wa Mbeya City kupitia Halmashauri ya jiji la Mbeya ulianza mchakato wake wa ununuzi wa usafiri kwa ajili ya timu mwaka jana na hatimaye sasa Basi hilo limeishawasili nchini.


Kwa mara ya kwanza Basi hilo limeonekana leo jijini Dar es Salaam na litakwenda jijini Mbeya wikiendi hii na litaanza kutumika baada ya timu kutoka kwenye mapumziko ya muda mfupi ya Ligi Kuu Bara.


Kwa maana hiyo City itaanza kulitumia Basi hilo Desemba 19 ambapo ligi itaanza tena. Tayari uongozi wa City umethibitisha ujio wa Basi hilo.


Post a Comment

 
Top