BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally.

WANASEMA ukistaajabu ya Musa basi utayaona ya firauni. Hebu angalia timu za jijini Tanga zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom mwenendo wao kwenye ligi hiyo, kuna timu tatu ambazo zote kwaujumla zimefunga mabao manne pekee mpaka sasa yaliyopatika kwenye mechi 19 walizocheza.

Kikosi cha Coastal Union


Timu hizo ambazo ni Coastal Union, African Sports na Mgambo JKT zimekuwa zikisuasua kwenye ligi hiyo kitu ambacho kinaashiria kwamba wakiendelea na mwenendo huo basi wanaweza kuwa kwenye hatari ya kushuka daraja hasa upande wa Coastal Union na African Sports.

Kikosi cha African Sports

Coastal ambayo ni moja ya timu kongwe za jijini Tanga kushiriki ligi hiyo imecheza mechi saba mpaka lakini haijafaunga bao hata moja huku ikishika nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi tatu ambazo walizipata akwenye sare za michezo mitatu.

Kikosi cha Mgambo JKT

Sports yenyewe inashika nafasi ya 14 ikiwa na pointi tatu ambazo walizipata kwenye mechi yao moja waliyoshinda dhidi ya Stand United huku Mgambo ikishinda mechi mbili, sare mbili na kukusanya pointi nane ambazo zimewaweka kwenye nafasi ya 10 katika msimamo wa ligi hiyo. African Sports na Mgambo wao wamecheza mechi sita kila mmoja.

Timu ambayo inashika mkia ni JKT Ruvu ya jijini Dar es Salaam ambayo haijashinda mechi hata moja huku ikiwa na pointi moja tu iliyopata kwenye mechi yao wsssaliyotoka sare

Post a Comment

 
Top