BOIPLUS SPORTS BLOG

IMERIPOTIWA kuwa kiungo wa Real Madrid Isco ameitaarifu klabu yake kuwa anataka kuondoka Santiago Bernabeu.

Muhispania huyo, ambaye amehusishwa na timu kadhaa za Ligi Kuu ya Uingereza, amemwambia rais wa Los Blancos, Florentino Perez kuwa anataka kujiunga na klabu nyingine kupata changamoto mpya kwa mujibu wa Daily Express.


Isco amekuwa akihaha kusaka nafasi kikosi cha kwanza Real Madrid tangu ujio wa Mateo Kovacic kutoka Inter Milan uhamisho wa majira ya joto na hajafunga katika mechi 14 alizocheza muhula huu.

Kiungo huyo anayekadiriwa kuwa na thamani ya euro milioni 35 inasemekana anatakiwa na Arsenal, Chelsea na Liverpool.

Post a Comment

 
Top