BOIPLUS SPORTS BLOG

LEO hii imetolewa listi ya wachezaji ambao jezi zao zinaongozwa kwa kuuza Ulaya, listi imetolewa na wa mtandao wa Kitbag.com na kuorodhesha majina ya wachezaji 10 ambao jezi zenye namba zao zinaongoza kwa kuuzwa barani ulaya.

Winga mpya wa klabu ya Manchester United anayevaa jezi namba 7, Memphis Depay amewashtua wengi baada ya kushika nafasi ya tatu nyuma ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo huku akiwa ndio mchezaji ambaye jezi zake zinauzika sana katika ligi kuu ya EPL.

Pamoja na kutokuanza vyema maisha yake ndani ya klabu yake ya United, Depay ameonekana kuwavutia wanunuzi wengi wa jezi barani Ulaya akiungana na wachezaji wenzake wawili wa United Wayne Rooney na Bastian Schweinsteiger katika 10 bora.
Eden Hazard, Alexis Sanchez, Aguero, na Coutinho ni wachezaji wengine wa EPL ambao wapo ndani ya Top 10.

ORODHA KAMILI IPO HIVI;
1) Lionel Messi – Barcelona
2) Cristiano Ronaldo – Real Madrid
3) Memphis Depay – Manchester United
4 Bastian Schweinsteiger – Manchester United
5) Eden Hazard – Chelsea
Rooney – Manchester United
7) Neymar – Barcelona
8) Sergio Aguero – Manchester City
9) Alexis Sanchez – Arsenal
10) Philippe Coutinho – Liverpool

Post a Comment

 
Top