BOIPLUS SPORTS BLOG

KIUNGO mpya wa Mbeya City, Haruna Moshi 'Boban'  amesema kikosi chake kina nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba itakayochezwa keshokutwa Uwanja wa Sokoine,  jijini Mbeya.

Boban amesema ana imani kubwa ya kupata ushindi katika mechi yake ya kwanza dhidi ya Simba baada ya kukitazama kikosi chake katika mazoezi yaliyofanyika leo uwanja wa Sokoine ambapo yeye ilikuwa ni mara yake ya kwanza tangu asajiliwe na kikosi hicho.

“Nimefanya mazoezi leo kwa mara ya kwanza na kikosi changu, hakika imekuwa siku nzuri kwangu, City ni timu bora na ina wachezaji vijana na wenye vipaji na uwezo mkubwa katika soka, naamini tutashinda mechi yetu dhidi ya Simba.

“Lengo langu ni moja tu kufanya kazi kwa nguvu ili kuisaidia timu kufanya  vizuri, naamini muda si mrefu kila mmoja atakuwa na kauli nyingine juu yangu na Mbeya City,” alisema Boban.

Kiungo mpya wa Mbeya City, Haruna Moshi 'Boban' akiwa na kipa Juma kaseja (kulia)


Hiyo pia itakuwa ni mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu tangu msimu huu uanze na tangu alipoachana na Coastal Union ya jijini Tanga.

Wakati huo huo, kipa wa City, Juma Kaseja amekiri kwamba mechi hiyo itakiwa ngumu kwake kwa madai kuwa mechi hiyo itakuzikutanisha  timu zenye sura mbili tofauti kwenye vikosi vyake.

“Kwangu mimi huu utakuwa mchezo mgumu, City tutaingia uwanjani tukiwa na rekodi nzuri mbele ya Simba huku pia kikosi chetu kikiwa na nyota vijana  wenye vipaji vikubwa ambao bado wana kiu kubwa ya kucheza na kudhihirisha ubora wao, hivyo sina shaka na sisi kupata ushindi, nafahamu Simba wamekuwa imara msimu huu na wameshinda michezo yao yote ya mwanzo, hilo halitunyimi nafasi ya ushindi hasa ukizingatia tutakuwa tunacheza kwenye Uwanja wetu wa nyumbani mbele ya mashabiki wetu. 

“Tumepoteza michezo minne  mpaka sasa hili ni deni kubwa kwa mashabiki wetu, tutacheza kufa na kupona ili kupata matokeo ni wazi utakuwa mchezo mgumu lakini nia yetu ni kushinda, tunazihitaji pointi tatu kutoka kwao siku hiyo, wao ni timu ngumu lakini sisi tuna kikosi kizuri,'' alisema Kaseja.

Post a Comment

 
Top