BOIPLUS SPORTS BLOG

MSHIRIKI wa Bongo Star Search (BSS), Kayumba Juma kutoka Dar es Salaam ameibuka mshindi wa shindano hilo lilifanyika usiku huu katika Ukumbi wa King Solomon Hall na kujinyakulia kitita cha Sh 50 milioni.

Mshindi wa pili katika shindano hilo ni Nassib Fonabo kutoka Arusha huku Frida Amani akiishia nafasi ya tatu.

Katika shindano hilo ni washiriki sita ndiyo waliofanikiwa kuingia kwenye fainali hiyo ambayo ilianza kwa michujo ya awali ambapo walishindana kwa hatua moja na kubaki washiriki watano walioingia tano bora huku Jacqline Kakenge kutoka Bukoba akitupwa nje.

Kampuni ya kutengeza simu ya Huawei ilitoa zawadi ya simu kwa washiriki wote walioingia sita bora.

Walioingia tano bora ni Nassib, Angel, Frida, Kayumba Juma na Kelvin Gerson ambao baadaye walichujwa na kubaki watatu.
Waliobaki hatua ya pili na kuingia hatua ya tatu bora ni Kayumba, Frida na Nassib huku Angel na Gerson  wakichapa lapa.

Shindano hilo lilisindikizwa na burudani ya muziki kutoka kwa wasanii mbalimbali ambao ni Ben Paul, Peter Msechu na Kala Jeremiah ambao ni matunda ya BSS, Yamoto Band, Navy Kenzo, Christian Bella na Rantana toka Nigeria


MC SizaMshehereshaji wa shughuli hiyo, Siza Daniel alitaka kuchafua hali ya hewa ukumbini hapo baada ya kutamka 'Hapa kazi tu' kauli ambayo hutumiwa na mgombea urais kwa tiketi ya CCM, John Pombe Magufuli ambapo watazamaji walianza kuonyesha ishara ya mabadiliko inayotumiwa na UKAWA.
Hata hivyo Mkurugenzi wa BSS, Madam Ritha alimtaka Siza kuachana na maneno ambayo hayahusiani na shughuli husika.

Wakati Ritha akimaliza kuelezea hilo baadaye alijikuta akitokwa na machozi baada ya mshiriki Kayumba kupanda na kuimba wimbo ambao ulionyesha umemgusa kutokana na uwezo wake mkubwa wa kumiliki jukwaa.

Post a Comment

 
Top