BOIPLUS SPORTS BLOGKOCHA MKuu wa Simba, Dylan Kerr amewaondoa hofu mashabiki wa timu hiyo kuhusu kumkosa mshambuliaji wao Hamisi Kiiza ambaye ni majeruhi ambapo ametamka kwamba Boniface Maganga ndiye atakayeiliza Mbeya City huku akimsifia beki wake Hassan Isihaka kuwa anastahili kuichezea Taifa Stars.

Kiiza ambaye ni Mchezaji Bora wa timu hiyo anasumbuliwa na nyama za paja ambapo atakosa mechi hiyo itakayochezwa Oktoba 17, Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Kerr ameiambia BOIPLUS kuwa wengi wana imani kubwa na Kiiza kwasababu amefunga mabao matano katika mechi zake alizocheza lakini yeye binafsi anaamini kwamba Maganga ni mchezaji mzuri na atamzidi kiwango Kiiza hapo baadaye.

''Najua mashabiki wa Simba wanataka kumuona Kiiza akicheza na ushawishi huo umeongezeka zaidi alipofunga mabao matano ila nataka kuwaambia kwamba Maganga atakuwa bora kuliko Kiiza.

''Maganga ana kipaji cha pekee na anafanya vizuri mazoezini na hata nikimpanga anaonyesha kiwango cha juu hivyo sina wasiwasi na mechi ijayo atacheza nafasi ya Kiiza na tutashinda,'' alisema Kerr

Akizungumzia kwa upande wa Isihaka alisema kuwa ''Mchezaji ukiona umeitwa kikosi cha timu yako ya Taifa ujue kuwa wewe unaweza hivyo ndivyo ninavyojivunia kwa Isihaka ambapo huitwa kila mara Stars,''.

Simba imeanza mazoezi yake ramsi leo kwenye Uwanja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ingawa kuna habari kwamba timu hiyo itaondoka Oktoba 10 kwenda jijini Mbeya ambako itapiga kambi ikisubiri mechi hiyo.

Post a Comment

 
Top