BOIPLUS SPORTS BLOG

MSHAMBULIAJI wa Simba, Hamisi Kiiza leo ametangazwa Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Vodacom wa mwezi uliopita na kuwapiki wenzake wawili, Elius Maguri na Amissi Tambwe.

Kiiza ambaye pia mwezi uliopita alikuwa Mchezaji Bora wa timu ya Simba na kujinyakulia kitita cha Sh 500000 na tuzo na sasa atapewa Sh 1 milioni kutoka kwa mdhamini wa ligi hiyo, Kampuni ya simu ya Vodacom.

Hata hivyo Kiiza ataendela kuwa nje ya Uwanja kwani anasumbuliwa na nyama za paja na atakuwa nje ya uwanja mpaka timu hiyo itakapokwenda mapumziko mafupi ya ligi yanayoanza mwezi ujao.

Kiiza tayari ameanza mazoezi mepesi ya kukimbia nusu Uwanja kwa dakika 20 alizopangiwa na daktari wa timu hiyo Yassin Gembe, Kiiza ameiambia BOIPLUS kuwa kitendo cha kukaa nje ya uwanja muda mrefu kinatibua mipango yake ya soka.

"Sijawahi kukaa nje ya uwanja muda mrefu namna hii, nasikitika nakosa mechi muhimu. Huu uwanja wa Sokoine ni mzuri sana kama sijacheza hapa nitacheza uwanja upi mwingine wa mkoani ambao ni mzuri.

''Bado nasikia maumivu na sitaki kuharakisha kucheza kabla sijapona vizuri nataka nipone ili nikirudi nakuwa na kasi mpya. Mechi ya kesho ni ngumu kwani Prisons wanata ushindi ila sisi tunahitaji kushinda kesho, kwenye ligi kila timu ni nzuri na ngumu,'' alisema Kiiza.

Kiiza ameisadia Simba kufanya vizuri kwenye mwezi huo, ikiwemo kufunga mabao matatu (hat trick) kwenye mechi dhidi ya Kagera Sugar aliwashinda washambuliaji wa timu za Stand United (Elias Maguli) na Yanga (Amisi Tambwe). Ndani ya mwezi Septemba ambapo zilichezwa raundi tano, Kiiza amefunga mabao matano.

Post a Comment

 
Top