BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally, Mbeya.

SIMBA imeona isiwe tabu baada ya kuona wanafunga mabao machache kwenye mechi zake wameamua kuanza mchakato wa usajili wa straika wa timu ya Taifa ya Uganda, Erisa Sekisambu.

Hiyo ni baada ya kuuangalia usajili wao kwa umakini na kugundua kuwa walichokifanya ni kusajili viungo wengi huku washambuliaji wakiwategemea zaidi Hamisi Kiiza na Musa Mgosi pamoja na Pape Nd'ew ambaye huanzia benchi.

Habari kutoka ndani ya Simba zinasema kuwa viongozi wa klabu hiyo wameanza mazungumzo na straika huyo ambayo yamefikia pazuri na kwamba anaweza kusainishwa mkataba mara tu usajili wa dirisha dogo ukifunguliwa.

''Ni kweli mpango na Mavugo (Laudit) ulikuwepo kwasababu mkataba wake na Vital'O unamalizika lakini huyu Erisa ndio mchakato wake ni kama umemalizika,'' alisema.

Kiongozi huyo aliiambia BOIPLUS kuwa endapo Erisa atasajiliwa basi kuna uwezekano mkubwa wa kuachana na Pape pamoja na mchezaji mwingine wa kigeni ambaye atampisha Raphael Kiongera anayemalizia mkataba wake wa mkopo katika timu ya KCB ya Kenya.

Simba kwasasa ipo jijini Mbeya ikijiandaa na mechi yao dhidi ya Prisons itakayochezwa keshokutwa Jumatano uwanja wa Sokoine.

Post a Comment

 
Top