BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally.

STRAIKA wa Stand United, Elius Maguli amefikisha mabao sita baada ya kuifungia timu yake mabao mawili kati ya matatu waliyoifunga Prisons.

Mechi hiyo imechezwa leo Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga ambapo Prisons imekubali kichapo cha mabao 3-0 na Jumatano wana kibarua dhidi ya Simba mechi itakayopigwa Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Maguli tayari amewapiku Hamisi Kiiza wa Simba na Donald Ngoma wa Yanga wenye mabao matano kila mmoja huku Amissi Tambwe wa Yanga na Kipre Tchetche wa Azam wakiwa na mabao manne kila mmoja wakati Atupele Green akiwa na mabao matatu.

Maguli alisajiliwa Stand msimu huu baada ya kocha wa Simba, Dylan Kerr kupendekeza straika huyo apelekwe kwa mkopo kwani hakuridhishwa na kiwango chake na hivyo kuamua kuvunja mkataba baada ya makubaliano ya pande zote mbili, Simba na Maguli.

Maguli ametua Stand kwa mkataba wa mwaka mmoja na amekuwa ndiye nyota wa timu hiyo iliyo chini ya Kocha Mfaransa Patrick Leiwig kwa kuifungia mabao mengi.

Post a Comment

 
Top