BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally.

STRAIKA wa Stand United, Elius Maguli, leo ametupia mabao mawili katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Majimaji katika mechi yao iliyochezwa Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga.

Kwa mabao hayo Maguli amefikisha idadi ya mabao nane huku akiwaacha wenzake Hamisi Kiiza kutoka Smba, Amissi Tambwe na Donald Ngoma (Yanga) wenye mabao matano kila mmoja.

Kipre Tchetche wa Azam yeye ana mabao manne akifuatiwa na Atupele Green wa Ndanda, Jeremiah Juma (Prisons) na Miraji Athuman (Toto Africans) ambao wana mabao matatu kila mmoja.

Maguli aliyesajiliwa Stand akitokea Simba ya jijini Dar es Salaam ameonekana kung'aa katika mechi zake nane alizocheza ns kuanza katika kikosi cha kwanza isipokuwa  mechi moja pekee ya Simba  aliingia akitokea benchi.

Kwasasa Maguli amekuwa mchezaji mwenye msaada mkubwa Stand United iliyochini ya kocha Patrick Leiwig na kujihakikishia namba kwenye kikosi cha kwanza, na huenda ndiye akawa mfungaji tegemeo wa kikosi hicho kinachodhaminiwa na Kampuni ya uchimbaji madini ya Accacia.

Post a Comment

 
Top