BOIPLUS SPORTS BLOG

MANCHESTER United ikiwa ugenini imelazimisha sare ya 1-1 kwaCSKA Moscow katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa wa kundi B.

Anthony Martial aliunawa mpira kwenye eneo la hatari kunako dakika ya 14 na kuipa CSKA Moscow penalti iliyopigwa na Roman Eremenko na kuokolewa na kipa David De Gea.

Hata hivyo United hawakusalimika, mpira uliookolewa na De Gea ukamkuta Seydou Doumbia aliyeujaza wavuni dakika ya 15.

Baada ya United kutawala mpira kwa muda mrefu bila mafanikio, kocha Luis van Gaal, akafanya mabadiliko mwanzoni mwa kipindi cha pili kwa kumtoa kiungo mkongwe Bastian Schweinsteiger na kumwingiza Marouane Fellaini, mabadiliko yaliyoleta uhai.

Kama vile hiyo haikutosha, dakika ya 64 Van Gaal akamtoa beki aliyepwaya Marcos Rojo nafasi yake ikichukuliwa na Daley Blind, dakika moja baadae United wakapata bao la kusawazisha.

Bao hilo likuja baada ya Antonio Valencia aliyepanda kuongeza mashambulizi kupiga krosi iliyomkuta Anthony Martial aliyepiga mbizi na kufunga kwa kichwa, hilo likiwa bao lake la kwanza la Champions League kwa Manchester United.

Katika mchezo mwingine wa kundi B Wolfsburg imeifunga PSV Eindhoven 2-0 na kuongoza kundi hilo, huku CSKA Moscow ikishika nafasi ya pili, United ya tatu na PSV ikishika mkia. 

Matokeo ya michezo mingine ya UEFA yanapatikana hapa.Post a Comment

 
Top