BOIPLUS SPORTS BLOG

By: Christian Simba


ANTHONY Martial ametajwa kuwa mchezaji bora wa mwezi kwa Septemba na Ligi Kuu baada ya kuwa na mafanikio ya haraka ndani ya Manchester United baada ya kujiunga mwishoni mwa dirisha la usajili.


Kinda huyo wa Ufaransa alijiunga Old Trafford akitokea Monaco kwa ada ya pauni milioni 36 na kufunga magoli matatu ndani ya mwezi.Juan Mata amepewa tuzo hiyo lakini na mashabiki kama mchezaji bora Septemba

Martial alitokea benchi na kufunga goli katika mechi yake ya kwanza dhidi ya Liverpool Old Trafford na kisha kufunga magoli mawili katika ushindi wa 3-2 dhidi ya Southampton.


Lakini Juan Mata amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Man U kwa mujibu wa kura za mashabiki. Naye kocha wa Tottenham Mauricio Pochettino ameshinda tuzo ya kocha bora wa Septemba.Post a Comment

 
Top