BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally, Mbeya.

YAKIWA yamebaki masaa 31 asubuhi ya leo, kabla mechi ya Simba na Mbeya City ichezwe, mshambuliaji mahiri Hamis Kiiza aliamua kuanza kufanya mazoezi na kikosi cha wekundu hao wa Msimbazi na huenda kesho akacheza mechi hiyo.


Tangu Simba waanze maandalizi ya mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara itakayochezwa Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, Kiiza hakuwahi kufanya mazoezi hayo kwani anasumbuliwa na nyama za paja.

Kocha Mkuu wa Simba, Dylan Kerr amesema kuwa bado hajaamua juu ya kumtumia mshambuliaji huyo mwenye mabao matano na kueleza kuwa kesho asubuhi ndiyo atakuwa na jibu sahihi.
Hata hivyo Kerr alisema ingawa hana uhakika wa mchezaji huyo kucheza ila afya yake kwasasa imeimarika ukilinganisha na hapo awali.

"Kiiza anaendelea vizuri na ndiyo maana ameanza mazoezi lakini sijaamua kama nitamtumia kesho au lah. Kesho asubuhi nitaangalia jinsi atakavyoamka ndipo nami nitakuwa na uamuzi," alisema Kerr.

Hata kama Kiiza hatacheza bado Kerr ana nafasi ya kuchagua mbadala wake ambapo imetajwa kuwa Boniface Maganga au Joseph Kimwaga ndiyo watakaocheza nafasi ya Kiiza.

Post a Comment

 
Top