BOIPLUS SPORTS BLOG

Uholanzi imeshindwa kufuzu mashindano ya Euro 2016 baada ya Robin van Persie kujifunga goli mwenyewe wakifungwa nyumbani na Jamhuri ya Czech iliyokuwa na wachezaji 10.

Uholanzi ilihitaji ushindi na Iceland ikiifunga Uturuki waweze kuingia kwa mlango wa nyuma (play-off), lakini Van Persie aliipatia Czech goli pamoja na mchezaji wao Mark Suchy kuonyeshwa kadi nyekundu.

Robin van Persie alijifunga mwenyewe dakika ya 66 na kuifanya Czech kuwa mbele kwa 3-0
Klaas-Jan Hunterlaar na Van Persie waliifungia Uholanzi lakini Pavel Kaderabek na Josef Sural nao waliifungia Uturuki na hivyo kushika nafasi ya tatu.

MATOKEO YA MECHI
NetheRland 2-3 Czech Rep
Wales 2 – 0 Andorra
Latvia 0 – 1 Kazakhstan
Turkey 1 – 0 Iceland
Belgium 3 – 1 Israel
Cyprus 2 – 3 Bos-Herze
Bulgaria 2 – 0 Azerbaijan
Italy 2 – 1 Norway
Malta 0 – 1 Croatia

Post a Comment

 
Top