BOIPLUS SPORTS BLOG

KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Boniface Mkwasa amesema kuwa matarajio yake ya jana ilikuwa ni kupata mabao mengi zaidi lakini kutokuwa makini kwa wachezaji wake kuliwafanya washindwe kuzitumia vizuri nafasi walizozipata hivyo kuwa na kibarua kigumu wakati wa mechi ya marudiano itakayochezwa Jumapili ya keshokutwa jijini Blantye, Malawi

Kauli hiyo ya Mkwassa iliungwa mkono na Nahodha wa Stars, Nadir Haroub 'Canavaro' ambaye amesema kuwa ushindi huo ni mkubwa kwao ila bado kazi yao ni ngumu ugenini.

Mkwassa alisema kwasasa anapaswa kufanyia kazi mapungufu aliyoyaona katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na Stars ilishinda bao 2-0, hivyo wanahitaji ushindi ama kutoka sare yoyote kwenye mechi ya marudiano ili wasonge mbele kucheza na Algeria.

"Tunashukuru tumeshinda mechi hii, kuna mapungufu nimeyoana ambayo nitayafanyia kazi kwani nilitaka mechi hii tufunge mabao mengi lakini tumebahatika kupata hayo mawili, bado nina kazi ya kusaka ushindi ugenini," alisema Mkwassa.

Kwa upande wa Canavaro alisema kuwa "Tumeshinda hapa ila bado tunahitaji kushinda pia ugenini ili tusonge mbele, Malawi ni timu nzuri, tumekutana nayo mara nyingi, hivyo hatutakiwi kuibeza kwa ushindi huu wa nyumbani, kazi bado ni ngumu mbele yetu ingawa tunaamini tutashinda,".

Post a Comment

 
Top