BOIPLUS SPORTS BLOG

SHIRIKISHO la Soka nchini (TFF) limempa mkataba mpya Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa amepewa mkataba wa mwaka mmoja na nusu ambao umeanza rasmi Oktoba Mosi na utamalizika Machi 31, 2017.

TFF imefikia makubaliano hayo na Mkwasa baada ya kuridhika na utendaji wake katika kukinoa kikosi cha Stars, ambapo mpaka sasa ameweza kuingoza Stars katika sare ya michezo miwili dhidi ya Uganda na Nigeria.

Kufuatia kusaini mkataba huo, Mkwasa atapatiwa huduma na marupurupu yote aliyokuwa akipewa kocha aliyeondoka.

Mkwassa ameeleza kufurahishwa na makubaliano haya na ameahidi kufanya kila jitihada kuhakikisha kiwango cha Taifa Stars  kinapanda.

Mkwassa ametoa wito kwa wadau wa mpira kumpa ushirikiano katika majukumu yake mapya.

Post a Comment

 
Top