BOIPLUS SPORTS BLOG

KOCHA Juma Mwambusi leo amesaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu kuifundisha Yanga ya jijini Dar es Salaam ambapo atakuwa Msaidizi wa Kocha Mkuu, Hans Pluijm.

Yanga imechukuwa hatua hiyo baada ya kocha wao wa zamani Boniface Mkwasa kupewa mkataba wa ajira wa kuifundisha Taifa Stars.

Baada ya dili hilo kukamilika kwa Mwambusi, jana aliamua kuwaaga wachezaji wa Mbeya City pamoja na viongozi wa klabu hiyo na leo amewasili jijini Dar es Salaam kumalizana na Yanga.

Habari kutoka ndani ya Yanga zinasema kuwa kesho Mwambusi atatambulishwa kwa wachezaji wao ambapo mechi yake ya kwanza kukaa kwenye benchi la ufundi ni dhidi ya Azam FC itakayochezwa Jumamosi katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
''Mwambusi amesaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu na ataanza kazi mara moja kwani tuna mechi ngumu mbele yetu, Mwambusi ni kocha mzuri na ana sifa zote ambazo Pluijm anazihitaji,'' alisema kiongozi huyo.

Mwambusi amewapiku makocha wenzake wawili ambao walikuwa kwenye mapendekezo ya Yanga, Felix Minziro na Mbwana Makatta.

Post a Comment

 
Top