BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
SIMBA huenda ikakosa huduma ya kiungo wao Justice Majabvi ambaye mkataba wake umebaki miezi miwili na yeye ametamka kuwa hakuna kiongozi yeyote aliyezungumza naye kuhusu kupewa mkataba mpya.

Majabvi amesema kuwa mkataba wake na Simba ulikuwa ni wa miezi sita ambapo ametumikia miezi minne na amebakiza miezi miwili pekee. Mzimbabwe huyo amekuwa na msaada mkubwa ndani ya kikosi cha Simba kutokana na juhudi zake binafsi hasa pale timu inapoelemewa.


"Mkataba wangu unamalizika, ni kweli sijafanya mazungumzo na viongozi wangu hivyo nawasilikilizia wao, mkataba wangu na Simba ni wa miezi sita tu, hivyo mpaka sasa umebaki wa miezi miwili," alisema Majabvi.

Hata hivyo habari zilizopatikana ni kwamba mchezaji huyo amechukizwa pia na kitendo cha kukalishwa hotelini tangu ajiunge na timu hiyo wakati makubaliano yao ya kimkataba ni kumpatia nyumba ya kuishi na familia yake jambo ambalo mpaka sasa halijatimia.


Majabvi ni chaguo la Kocha Mkuu, Dylan Kerr ambaye alipendekeza mchezaji huyo asajiliwe baada ya kuridhishwa na kiwango chake kwenye majaribio, Majabvi ana nafasi kubwa ya kupewa mkataba mwingine na kubaki Simba kwani ameonyesha kuwa na mchango mkubwa ndani ya Simba na ni mmoja wa wachezaji ambao wamekubalika kutokana na uwezo wake huo pamoja na kujitambua.

Post a Comment

 
Top