BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally.

MCHEZAJI wa zamani wa Yanga na African Sports, Nsa Job leo ameruhusiwa kutoka hospitali  ya KCMC Moshi alikokuwa amelazwa baada ya kuumizwa kichwani walipovaniwa na kupigwa na kitu kilichodaiwa kuwa ni jiwe wakiwa  wametoka kwenye kampeni.

Nsa Job


Ilielezwa kwamba Nsa alitoka kwenye kampeni za mmoja wa wagombea wa ubunge kwa tiketi ya CCM huku ikidaiwa vurugu hizo zilitokea kati ya wanachama  wa vyama vya upinzani vinavyounda Umoja wa  Katiba ya Wananchi (UKAWA) na wale wa CCM.


Nsa aliumizwa kichwani na kupoteza fahamu na kupelekea kulazwa ICU na kufanyiwa upasuaji wa kichwa ambapo leo ameruhusiwa rasmi kutoka hospitali.


Mwenyezi Mungu aendelee kumpigania Nsa ili apone kabisa.

Post a Comment

 
Top