BOIPLUS SPORTS BLOGKOCHA wa Stars Charles Boniface Mkwasa aliyelamba shavu jipya jana kwa mkataba wa miezi 18 ametaja 'majembe' 11 yatakayoanza kuitetea Tanzania katika mchezo wa leo dhidi ya Timu ya taifa ya Malawi 'The Flmes'. Mchezo utachezwa katika dimba la Taifa jijini Dar Es Salaam.

Mkwasa ameendelea kumuamini Ally Mustafa 'Barthez' kusimama katikati ya milingoti mitatu ya goli huku alindwa na Shomari Kapombe atakayecheza kama beki wa kulia na Haji Mwinyi atakayesimama upande wa kushoto. Walinzi wa kati ambao wanacheza pamoja kwenye klabu ya Yanga Nadir Haroub na Kevin Yondan, bado wameendelea kuaminiwa na 'Boss' wao huyo wa zamani.

Himid Mao atacheza kama kiungo mkabaji akishirikiana na Said Ndemla ambaye atakuwa akisukuma mashambulizi mbele. Straika mwenye nguvu wa Tp Mazembe Thomas Ulimwengu atakuwa akishambulia akitokea upande wa kulia mwa uwanja na kinda wa Azam Fc Farid Mussa atashambulia akitokea upande wa kushoto.

Mrisho Ngassa atakuwa pembeni mwa straika mwingine wa TP Mazembe mwenye mabao sita kwenye ligi ya mabingwa Afrika, Mbwana Samatta 'Samagoal' kuhakikisha Stars inapata mabao mengi iwezekanavyo.

Kitaalamu timu hii imepangwa kwa lengo la kushambulia sana na kupata mabao mengi ili kuweka urahisi kwenye mchezo wa marudiano utakaopigwa Malawi baadae. 

Post a Comment

 
Top