BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally, Mbeya.

SIMBA leo imefanya mazoezi yake ya mwisho kuelekea mechi yao ya  Ligi Kuu Bara dhidi ya Prisons itakayochezwa kesho kwenge Uwanja wa Sokoine na huenda kocha Dylan Kerr atamuanzisha straika wake Pape N'daw baada ya Musa Mgosi kuumia mguu.

Pape N'daw

Msenegal huyo hajawahi kuanza mechi hata moja na zaidi huanzia benchi na kupewa dakika zisizozidi 25 na hii itakuwa mara yake ya kwanza kucheza kikosi cha kwanza.

Kerr amesema kuwa Mgosi hajafanya mazoezi mpaka mwisho kwasababu mguu ulikuwa unamuuma ambapo Mgosi amesema amepatwa na malengelenge ya mguu kitokana na kiatu alichokuwa amevaa ila ana uwezo wa kucheza hapo kesho.

Kerr ameanza kuingiwa na uoga huo na hivyo kumwandaa Pape kama itashindikana kabisa kumtumia Mgosi ambaye uhakika wake utapatika kesho asubuhi.

"Nataka ushindi mechi ya kwanza tulicheza vibaya hivyo nimewaambia wachezaji wangu wajitume na kuhakikisha tunachukuwa pointi. Mgosi ana maumivu ya mguu ila nitaangalia hali yake kesho asubuhi,'' alisema Kerr.

Mechi hiyo itachezwa kesho Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya ambapo Simba wataingia na kumbukumbu nzuri ya kuvunja mwiko baada ya kuifunga Mbeya City bao 1-0 wakati Prisons wao walipoteza mechi yao dhidi ya Stand United ilikubali kichapo cha bao 3-0 hivyo wanaingia wakihitaji ushindi wa nyimbani.

Post a Comment

 
Top