BOIPLUS SPORTS BLOG

NYOTA wa Real Madrid, Christiano Ronaldo, leo amekabidhiwa tuzo yake ya kiatu cha dhahabu " Golden Shoe" na kumfanya awe mchezaji wa kwanza kuchukua tuzo hiyo mara 4.

Ronaldo amepewa kiatu hicho cha dhahabu baada ya kufunga jumla ya mabao 48 katika ligi kuu nchini Hispania La Liga katika msimu wa 2014/2015.

Tuzo hii hupewa mchezaji ambaye amefunga mabao mengi katika ligi kuliko wachezaji wengine katika ligi mbalimbali barani Ulaya.

Mara ya kwanza Ronaldo kuchukua tuzo hii ilikuwa msimu wa 2007/2008 akiwa Manchester United alipofunga mabao 31 katika EPL na alipohamia Real Madrid akachukua tuzo hiyo msimu wa 2010/2011 kwa mabao 40, 2013/2014 akifunga mabao 31 na 2014/2015 akifunga mabao 48 katika ligi hiyo ya La Liga.

Post a Comment

 
Top