BOIPLUS SPORTS BLOG

STRAIKA wa TP Mazembe ya DR Congo na timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', Mbwana Samatta ametajwa  katika orodha ya wachezaji 24 wanaowania tuzo ya Mchezaji Bora anayecheza Afrika.

Katika msimu uliopita, Samatta ambaye kwasasa ndiye straika wa kutumainiwa wa Mazembe, aliiwezesha timu yake hiyo kubeba ubingwa wa Ligi Kuu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) huku pia akiipeleka hadi nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Hii ni mara ya tatu kwa Samatta kutajwa katika tuzo hii inayotolewa na Shirikisho la soka barani Afrika (CAF). Akizungumza na BOIPLUS jioni ya leo kutokea Malawi alikoiongoza Stars kuiondoa Malawi kwenye hatua za awali za kufuzu Kombe la Dunia 2018 kwa jumla ya mabao 2-1, Samatta alisema kuwa anafarijika kuona anatajwa kwa mara ya tatu katika orodha ya wachezaji waowania tuzo hiyo.

"Kwa kweli najisikia faraja sana kwani ni mara ya tatu natajwa tangu nije Mazembe, hii inaonyesha ni kiasi gani Afrika inatambua uwezo wangu. Hii inaniongezea kujiamini na kwamba nitaingia katika soka la ulaya nikiwa ni mmoja kati ya wachezaji bora toka Afrika,'' alisema Samatta.

Samatta ambaye atamaliza mkataba wake na Mazembe mapema mwakani, amegoma kuongeza mkataba mpya na kwamba sasa akili na mawazo yake yote yapo Ulaya.

Post a Comment

haji chimbenga said... 14 October 2015 at 07:04

nani anapiga kura kwa hawa wachezaji?

 
Top