BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally, Dar
SIMBA leo imeifunga Coastal Union bao 1-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam wakati Yanga wao wakilazimisha sare ya mabao 2-2 dhidi ya Mwadui FC.

Mabao yote ya  Yanga yalifungwa na Donald Ngoma wakati mabao ya Mwadui yalifungwa na Paul Nonga na Fabian Gwande.

Kwa matokeo hayo Yanga imeendelea kubaki kileleni ikiwa na pointi 20 huku Simba wakifikisha pointi 18 Azam wao watacheza kesho wakiwa na pointi 19 mkononi.

Mfungaji wa bao pekee la Simba, Hamis Kiiza

Simba ndiyo ilikuwa ha kwanza kupata bao kupitia kwa mshambuliaji wake Hamisi Kiiza katika kipindi cha kwanza akipokea krosi ya Hassan Kessy.

Wachezaji wa Coastal Union, Abasirim Chidiebere na Ibrahim Twaha walikosa mabao ya wazi huku Said Ndemla naye akikosa bao kwani shuti lake alilopiga lilitoka nje kidogo ya goli.

Mwamuzi wa mchezo huo Jonesia Rukya alitoa kadi za njano kwa wachezaji wa Coastal Union, Hamad Juma, Yusuph Ssabo na Adeyun Saleh kwa kuwachezea rafu wachezaji wa Simba huku Jonas Mkude na Juuko Murshid nao wakizawadiwa kadi za njano.

Kocha wa Coastal, Jackson Mayanja alianza kufanya mabadiliko katika kipindi cha kwanza ambapo aliwatoa Ibrahim Twaha na Nasoro Kapama nafasi zao zilichukuliwa na Juma Mahadhi pamoja na Said Jailan wakati Dylan Kerr aliwatoa Kiiza na Peter Mwalyanzi nafasi zao zilichukuliwa na Ibrahim Ajibu na Mussa Mgosi.

Hata hivyo mabadiliko aliyoyafanya Kerr hayakuleta matokeo yoyote ya maana kwani pamoja na ushindi wa pointi tatu kikosi chao kimecheza chini ya kiwango.

Post a Comment

 
Top