BOIPLUS SPORTS BLOG

SIMBA inajiandaa na mechi yake ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbeya City, ambapo itamkosa beki wake wa kulia Hassan Kessy ambaye ana kadi tatu za njano lakini pia imepata pigo lingine kwani mbadala wa Kessy, Mrundi Emiry Namubona ameumia kidole cha mkononi na atakuwa nje kwa wiki nne.

Kwa mujibu wa ataarifa iliyotumwa na Msemaji wa Simba, Haji Manara ilieleza kuwa Emiry amevunjika kidole na hivyo atalazimika kuwa nje ya uwanja kwa wiki nne. Njia pekee ya Kocha wa Simba, Dylan Kerr anayoweza kuitumia ni kubadilisha mfumo ili kupata ushindi huo wa ugenini kwa kumchezesha Simon Sserunkuma kama beki wa kulia ambaye atakuwa na jukumu la kupanda na kushambulia.

Kwa upande wa mchezaji mwenyewe amesema kuwa "Nimeumia jana asubuhi mazoezini ambapo nimevunjika kabisa mfupa wa kidole, nimeambiwa nitakaa nje ya uwanja kwa mwezi mzima ingawa naamini kabla ya huo mwezi nitakuwa nimeanza mazoezi mepesi.
"Nilikuwa na hamu ya kucheza mechi hiyo ya Mbeya City lakini sitacheza mechi zote za mzunguko wa kwanza kwani kidole kitakuwa hakijapona," alisema Emiry.

Emiry atakosa mechi ya Mbeya City, Prisons, Coastal Union, Majimaji na Azam FC ambayo itakuwa ya mwisho na timu kwenda kwenye mapumziko ambapo mzunguko wa pili utaanza Desemba 19 Simba ikianza na  Toto Africans ya jijini Mwanza mechi itakayochezwa uwanja wa CCM Kirumba.

Post a Comment

 
Top