BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally, Mbeya.

Mchezaji wa Simba, Justice Majabvi akimtuliza Jumanne Alfadhili wakati akitaka kupigana na Pape N'dew wa Simba hayupo pichani

SIMBA ilishinda mechi iliyopita dhidi ya Mbeya City huku leo ikiambulia kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Prisons ya jijini Mbeya katika mechi ya Ligi Kuu iliyochezwa Uwanja wa Sokoine.

Simba iliingia uwanjani ikijiamini kuwa itaondoka na pointi sita kwa mechi zote mbili lakini imekuwa tofauti kwao kwani inarudi jijini Dar es Salaam ikiwa imekusanya pointi tatu tu.

Bao pekee la Prisons lilifungwa na Mohamed Mkopi dakika ya 62 akifunga kwa kichwa ikiwa ni krosi ya Jeremiah Juma huku kipa wa Simba Vincent Angban akishindwa kuokoa.

Mchezo huo haukuwa na mshambulizi yenye madhara hasa kwa upande wa Simba na kujikuta wanamaliza dakika 90 bila kusawazisha bao hilo lililowapa ushindi Prisons.

kipa wa Tanzania Prisons Aron Kalambo akiwania  mpira mbele ya mchezaji wa Simba, Pape N'dew (kushoto)  na beki wa Prisons James  Mwasote

Kocha wa Simba Dylan Kerr alikibadilisha kikosi chake cha leo ambapo aliwapumzisha Abdi Banda, Jonas Mkude ambao hawakuwepo hata benchi huku Peter Mwalyanzi na Pape N'dew wakianza kikosi cha kwanza.

Kerr alifanya mabadiliko katika kikosi cha ambapo alimtoa Awadh Juma na Simon Sserunkuma, Mwalyanzi na kuwaingiza Mwinyi Kazimoto, Ibrahim Ajibu na Said Ndemla huku kocha wa Prisons naye akiwatoa Benjamin Asukile, 

Mohamed Mkopi ambapo nafasi zao zilichukuliwa na Leonsi Mutalemwa na Ally Manzi.
Mwamuzi wa mchezo huo Jimmy Fanuel  pia alitoa kadi za njano wachezaji wa Prisons ambao ni kipa Aron Kalambo na Kijiko aliyemchezea rafu mchezaji wa Simba.

Simba inaanza safari kesho ya kurudi jijini Dar es Salaam kujiandaa na mechi nyingine ikiwa imekusanya pointi 15 huku Yanga wenyewe wakiendelea kujiimarisha kileleni ikiwa na pointi 19 baada ya kuifunga Toto African bao 4-1.

Post a Comment

 
Top