BOIPLUS SPORTS BLOG

KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Boniface Mkwasa amesema kikosi chake kipo tayari kwa mchezo wa kesho dhidi ya Malawi kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia 2018.

Mkwasa amesema kikosi chake kipo katika hali nzuri baada ya kufanya mazoezi ya mwisho leo asubuhi ambapo wachezaji wote wakiwemo wachezaji wawili Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu kutoka klabu ya TP Mazembe ya DR Congo.

“Tunatambua umuhimu wa mchezo wa kesho, wachezaji wana ari na morali ya hali ya juu, kikubwa tunawaomba watanzania wajitokeze kwa wingi uwanjani kuja kutu sapoti katika mchezo huo,” alisema Mkwasa.

Kwa upande wa Kocha Msaidizi wa Malawi 'The Flames', Ramadhan Nsanzurwimo amesema wanaiheshimu Tanzania, wanatambua kesho kutakuwa na mchezo mzuri, na wao wamejiandaa vizuri kwa mchezo huo.

Post a Comment

 
Top