BOIPLUS SPORTS BLOG

TAIFA Stars imefanikiwa kusonga hatua ya pili ya michuano ya kufuzu kushiriki Kombe la Dunia 2018 baada ya kuindoa Malawi 'The Flames'.

Katika mechi ya awali iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Jumatano ya wiki hii jijini Dar es Salaam, Stars ilishinda bao 2-0 ambapo mechi ya marudiano iliyochezwa jioni ya leo Uwanja wa Kamuzubanda Stars imekubali kichapo cha bao 1-0. Bao la Malawi limefungwa na John Banda dakika ya 43.

Katika mchezo huo wachezaji wa Stars, John Bocco, Farid Musa, Mudathir Yahya, Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta walipewa kadi za njano wakati Malawi waliopata kadi za njano ni Limbikani Mzava na Kuwali.

Kocha wa Stars, Boniface Mkwasa, alifanya mabadiliko ambapo aliwatoa Said Ndemla na Farid Mussa na kuwaingiza Bocco na Mrisho Ngassa. Malawi wao walimtoa Gerald Phiri, Micium Mhone na Miracle Gabeya nafasi zao zilichukuliwa na Isaac Kaliati, Gabadinho Mhango na Robin Ngarande.

Stars imeitoa Malawi kwa jumla ya bao 2-1 sasa itajiandaa  kucheza na Algeria.

Post a Comment

 
Top