BOIPLUS SPORTS BLOGKIKOSI cha Taifa Stars  kimewasili salama katika Mji wa Blantyre nchini Malawi jioni ya leo tayari kwa mchezo wa marudiano siku dhidi ya wenyeji siku ya Jumapili.

Stars inayonolewa na makocha wazawa Boniface Mkwasa na Hemed Morocco iliondoka leo kwa usafiri wa shirika la ndege la Fastjet na kuwasili jiji la Lilongwe saa 4 asubuhi kabla ya kuanza safari ya Basi kuelekea Blantyre iliyochukua takribani saa tatu.

Wachezaji wote wapo katika hali nzuri kuelekea katika mchezo wa marudiano ambapo Stars itashuka dimbani kusaka matokeo mazuri yatakayoiwezesha kufuzu kwa hatua ya pili, katika mchezo wa awali  uliochezwa jijini Dar es salaam, Stars iliibuka na ushindi wa mabao 2- 0.
Stars inatarajiwa kufanya mazoezi kesho jioni katika Uwanja wa Kamuzu Banda uliopo Blantyre, Uwanja ambao utatumika kwa mchezo huo.

Kuelekea mchezo huo wa marudiano, Mkwasa amesema vijana wake wote wapo katika hali nzuri kiafya, kifikra na morali ni ya hali ya juu kuelekea kwenye mchezo huo.
Katika hatua nyingine mabasi mawili yenye washabiki wa 'Stars Supporter' yako njiani kuelekea nchini Malawi kwa ajili ya kuipa sapoti Stars katika mchezo huo.

Post a Comment

 
Top