BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Karim Boimanda.


MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba, Uhuru Seleman juzi aliipatia timu yake bao la kusawazisha katika mechi ya Ligi Daraja la Kwanza nchini Afrika Kusini (NFD) na kuifanya timu yake itoke sare ya bao 1-1 dhidi ya Thanda Royal Zulu Fc.

Mechi hiyo ilichezwa Uwanja wa King Zwelithini jijini Durban ambapo tayari Uhuru anayeichezea Royal Eagles kwa mkopo akitokea Jomo Cosmo amefikisha mabao matatu.

Uhuru amefunga mabao hayo katika mechi tano alizocheza, mechi nne ametokea benchi na moja ameanza.

Uhuru ameonyesha kupambana kuhakikisha anapata namba kikosi cha kwanza na tayari ameanza kumshawishi kocha wake kwa mechi alizocheza na kuonyesha kiwango cha juu.


Post a Comment

 
Top