BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally.
KOCHA Mkuu wa Toto Africans ya jijini Mwanza, Martin Grelics amejiuzulu kuifundisha timu hiyo na tayari juzi aliwaaga wachezaji wake.

Grelics alijiunga na Toto msimu huu wa Ligi Kuu Bara lakini imeelezwa kuwa mazingira magumu aliyokutananayo katika klabu hiyo yamemfanya ashindwe kufanyakazi yake kwa ufanisi.


Habari kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema kuwa kocha huyo atamalizia kufundisha mechi mbili tu  zilizobaki za ligi kabla ya kwenda kwenye mapumziko mafupi.

''Ni kweli kocha alituaga tangu juzi Jumamosi kuwa tutakaporudi kutoka kwenye mapumziko mafupi hatutakuwa naye. Kuna mambo mengi yanaendelea ikiwemo wachezaji kutolipwa mishahara yao pamoja na mfumo mbovu wa viongozi ndiyo maana ameshindwa kukaa zaidi,'' kilisema chanzo hicho.

Katika barua ya kocha huyo aliyowaandikia viongozi wa Toto ilitaja vikwazo vingi vya ufanisi wa kazi yake huku akisisitiza katika tatizo la wachezaji wake kutolipwa mishahara pamoja na kitendo cha timu kufanya mazoezi ya pamoja mara sabu tu katika mwezi uliopita.


Kocha huyo atakapoondoka  kikosi hicho kitaongozwa na kocha mzawa John Tegete ambaye ni kocha msaidizi mpaka hapo watakapompata kocha mkuu mwingine.

Post a Comment

 
Top