BOIPLUS SPORTS BLOG

HATIMAYE Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ni kama amejirudi baada ya kutamka wazi kuwa, anajiandaa kumsajili mshambuliaji wa Paris Saint – Germain ya Ufaransa, Edinson Cavani.

Wenger ambaye amekuwa mbishi linapokuja suala la kutoa fedha nyingi kununua wachezaji, kwa sasa amenyooka na amesema yuko tayari kumwaga fedha katika usajili wa dirisha dogo.

Alifichua kuwa staa huyo aliyeshindwa kung’aa akiwa na Paris Saint-Germain amekuwa shabaha yake kuu.

“Nimekuwa nikimfatilia Cavani kabla hajaenda PSG lakini tulilazimika kuachana nae baada ya dau lake kupanda,” alisema.

Imeelezwa kuwa Wenger amejitosa kwa Cavani baada ya kukithiri kutoelewana kwa mchezaji huyo na Kocha wa PSG, Laurent Blanc.

Aidha, Wenger amesema anataka kusajili wachezaji watatu wapya wa kiwango cha dunia, huku akipambana kuizuia Real Madrid isimsajiri kinda wake Dani Ceballos mwenye miaka 19

Post a Comment

 
Top