BOIPLUS SPORTS BLOG

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga wamerudi katika nafasi yao ya juu baada ya kuifunga Kagera Sugar bao 2-0 katika mechi iliyochezwa Uwanja wa Alli Hassan Mwinyi, Tabora.

Yanga ilishushwa kileleni na Azam Fc na hivyo imepanda baada ya kufikisha pointi 23 huku Azam wakiwa na pointi 22 sawa na Mtibwa 
wakati Simba wao wanashika nafasi ya nne kwa kufikisha pointi 21.


Yanga na Simba zimecheza mechi tisa kila moja wakati Azam wao wàmecheza mechi nane huku wakiwa na kibarua dhidi ya Toto Africans ya jijini Mwanza mechi itakayochezwa kesho Uwanja wa Chamazi.

Mabao ya Yanga yalifungwa na Donald Ngoma dakika ya 23 na hivyo kufikisha mabao nane sawa na Elius Maguli wa Stand United na Hamisi Kiiza wa Simba ambao pia wana mabao nane kila mmoja. Bao la pili lilifungwa na Deus Kaseke ikiwa ni dakika ya 62.

Mbeya City wao wametoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Coastal Union mechi iliyochezwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Post a Comment

 
Top