BOIPLUS SPORTS BLOG

KWA mara nyingine tena, Arsenal imeshindwa kukaa juu ya msimamo wa Ligi Kuu Uingereza pale iliporuhusu kipigo cha bao 2-1 kutoka kwa West Bromwich Albion.


Arsenal itabidi ijilaumu yenyewe kwa kushindwa kuambulia japo sare baada ya kiungo Santi Cazorla kukosa penalti dakika ya 84.

Ni Arsenal waliokuwa wa kwanza kupata goli dakika ya 28 kupitia kwa mshambuliaji Olivier Giroud aliyefunga kwa bao tamu la kichwa ambalo lilidumu kwa dakika nane tu kabla ya James Morrison kufunga kwa shuti kali dakika ya 35.


Dakika tano baadae Arsenal waliokuwa ugenini, wakaruhusu bao la pili lililokuja kwa njia ya kujifunga kupitia kwa kiungo Mikel Arteta. Kipigo hicho kimeiporomosha Arsenal hadi nafasi ya nne.

West Brom: Myhill 6.5; Dawson 7, Evans 7, Olsson 7.5, Brunt 7; Yacob 7, Fletcher 7; Sessegnon 6 (Gardner 61’ 5), Morrison 7 (Lambert 77’ 5), McClean 6.5; Rondon 6 (Berahino 68’ 6)

Arsenal: Cech 6; Bellerin 6, Mertesacker 6, Koscielny 6, Monreal 6; Coquelin 5 (Arteta 14’ 3 (Flamini 48’ 5), Cazorla 6; Sanchez 6, Ozil 6, Gibbs 5 (Campbell 63’ 4); Giroud 7


Post a Comment

 
Top