BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
VINARA wa Ligi Kuu Bara, Azam FC wamepania kuwavua ubingwa wa ligi hiyo Mabingwa watetezi Yanga kwa kudai kuwa sasa wataendelea kuongoza usukani japokuwa hawajapishana kwa pointi nyingi.

Kocha Mkuu wa timu hiyo, Stewart Hall amesema kuwa ingawa hawajapishana pointi nyingi na Yanga lakini bado dhamira yake ni kurudisha ubingwa huo Chamazi ambao walipokonywa na Wanajangwani hao.


Hall alisema kuwa ametoa mapumziko kwa wachezaji wake kwasababu kikosi chake kina wachezaji 10 wanaozichezea timu zao za mataifa mbalimbali hivyo wataanza kambi yao Novemba 23 wakati Yanga ambao pia wamepania kutetea ubingwa huo wametoa wiki moja tu ya mapumziko kwa wachezaji ambao hawapo kwenye vikosi vya timu za Taifa.

''Nataka kutwaa ubingwa na hilo ndilo lengo langu pekee kwenye msimu huu wa ligi. Nafahamu ligi ni ngumu na tunafukuzana na Yanga pale juu kwa pointi chache ila nitahakikisha tutakapoanza kambi ni kukijenga vizuri kikosi.

''Huwa naheshimu ninapocheza na timu kama Simba ama Yanga maana ni timu kubwa na zina mashabiki wengi. Ili nichukuwe pointi tatu katika mechi yetu na Simba basi ni kuhakikisha naimarisha kikosi zaidi,'' alisema Hall.

Post a Comment

 
Top