BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
BEKI wa Simba, Miraji Adam anatarajia kujiunga na Coastal Union ya jijini Tanga kwa mkopo wa miezi sita baada ya Simba kishindwa kuvunja mkataba wake.

Akizungumza na BOIPLUS, Miraji alisema kuwa amekubali kwenda huko baada ya kuona amekaa nje kwa muda mrefu pasipo kupata ufumbuzi wa kucheza jambo ambalo ni hatari kwani linaweza kumshusha kiwango chake cha soka.Miraji alisema kuwa anakwenda Coastal kucheza na kuisaidia timu hiyo katika Ligi Kuu Bara na mambo mengine yatafuata baada ya mkataba wake kumalizika hapo mwakani.

''Nimekaa nje muda mrefu baada ya Simba kushindwa kuvunja mkataba wangu na sasa wamenipeleka kwa mkopo Coastal Union jambo ambalo nisingeweza kukataa. Nataka kumalizia mkataba wangu ndipo nijue mengine.

''Mpira ndiyo ajira yangu hivyo ni lazima nijitume kuhakikisha narudi katika kiwango changu cha mwanzo, naweza kusema Coastal ni mahali pazuri kwangu,'' alisema Miraji

Awali Simba walimpeleka Miraji kwa mkopo katika timu ya Mtibwa Sugar ambapo hakupata nafasi ya kucheza na msimu uliopita ulipomalizika waliamua kumrejesha Simba.

Post a Comment

 
Top