BOIPLUS SPORTS BLOG
FRIEND Rangers jana walifanikiwa kurudi kileleni baada ya kulazimisha sare tasa na Kiluvya United, mechi iliyochezwa Uwanja wa Mabatini, Mlandizi. 

Kipindi cha kwanza timu zote zilicheza kwa kushambuliana kwa zamau na kwenda mapumziko huku hakuna aliyeweza kuona lango la mwenzake kwani timu zote mbili hazikuwa makini katika safu ya ushambuliaji ambao walishindwa kutumia vyema nafasi za kufunga walizokuwa wakipata.

Kipindi cha pili kilipoanza Rangers walionekana kubadilika na kuliandama zaidi lango la wapinzani wao na dakika ya 58 alikosa bao baada ya beki wa Kiluvya kufanikiwa kuondosha hatari langoni kwao ambalo lingesababisa wafungwe.

Hata hivyo Rangers iliendelea kulisakama lango la wapinzani wao ambapo mshambuliajia wao kaubutua  Khalid Badra alipiga shuti lililotinga nyavuni lakini refa alikataa kwa madai kwamba mfungaji aliunawa mpira. Dakika ya 65 Ranges walimtoa Yusufu Mgwao nafasi yake ilichukuliwa na Cliff Buyoya ambae aliongeza uhai sana kwenye mashambulizi lakini mpaka mpira unamalizika hakuna aliyeweza kuona lango la mwenzake.

Kwa matokeo hayo Rengers wanafikisha poin 11 sawa na Ashanti lakini Rangers wanaongoza kwa magoli yao matano huku Ashanti wakifuatia kwa pointi 11 lakini wana magoli matatu.

Post a Comment

 
Top