BOIPLUS SPORTS BLOG


Picha kwa hisani ya Futaa.com

BAADA ya kukwama kwa zaidi ya saa tisa katika Uwanja wa Ndege wa Wilson, hatimaye timu ya taifa ya Kenya 'Harambee Stars' wameondoka kuelekea Cape Verde katika Jiji la Praia kwa ajili ya mchezo wa kesho wa kuwania kufuza kwa michuano ya Kombe la Dunia 2018.

Harambee walikuwa waondoke saa nne asubuhi lakini kushindwa kwa Shirikisho la Soka nchini Kenya (FKF) kulipia  gharama za ndege zilisababisha kuchelewa kuanza kwa safari hiyo.

Wachezaji wa Harambee watalazimika kujiweka sawa baada ya kusafiri angani kwa zaidi ya saa nane kuanzia muda huu ili waweze kulinda ushindi wao wa bao 1-0 walioupata juzi jijini Nairobi.

Kenya iliichapa Mauritius kwa jumla ya mabao 5-2 katika hatua ya awali ndipo walipangiwa kucheza na Cape Verde watakaopaswa kupigana nao kufa kupona ili waingie hatua ya makundi ya kufuzu fainali hizo.

Post a Comment

 
Top