BOIPLUS SPORTS BLOG


JAMHURI ya Kidemokrasia ya Congo imepata ushindi wa 3-2 dhidi ya jirani zao Burundi kwenye mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia nchini Urusi 2018 iliyochezewa mjini Bujumbura.

Katika mechi hiyo iliyochezewa uwanja wa Prince Louis Rwagasore, DR Congo walianza mechi vyema kwa kufunga dakika ya tano kupitia kwa Yannick Bolasie.

Lakini Burundi walijikakamua na kukomboa bao hilo kupitia Cedric Amissi dakika ya 38 na timu zikaenda mapumzikoni zikiwa zimetoshana nguvu.
Kipindi cha pili, vuta nikuvute iliendelea lakini mambo yalifanyika dakika 10 za mwisho.

Burundi ndio walioanza kutisha katika dakika ya 83 kupitia Amissi tena, lakini mambo yalikuwa bado kuifanya Burundi iondoke kifua mbele.

Katika kipindi cha dakika mbili, Ndombe Mubele alifunga mabao mawili, dakika ya 86 na dakika ya 88, na kuwawezesha DR Congo kuondoka na ushindi.

Kwenye mechi nyingine, Guinea walilaza Namibia 1-0, Benin wakaishinda Burkina Faso 2-1 nao Uganda wakatia mkobani ushindi wa bao moja bila dhidi ya Togo.

Farouq Miya alifungia Cranes muda mfupi kabla ya mapumziko. Katika mchezo huo kipa Dennis Onyango aliokoa mkwaju wa penalti kutoka kwa Mathieu Dossevi.

Kwa kiasi Fulani, Uganda wameweza kulipiza kisasi cha kufungwa mara mbili na Togo kwenye mechi za kufuzu kwa Kombe la Taifa Bingwa Afrika 2015.

Mechi ya marudiano itachezewa Kampala Jumapili.

Yafuatayo ndiyo matokeo kamili ya mechi zilizochezwa jana:
Burundi 2-3 Congo DR
Namibia 0-1 Guinea
Benin 2-1 Burkina Faso
Togo 0-1 Uganda

Matokeo ya juzi yalikuwa
Msumbiji 1-0 Gabon
Sudan 0-1 Zambia

Post a Comment

 
Top