BOIPLUS SPORTS BLOG

MWENYEKITI wa Kamati Taifa Stars, Farough Baghozah amewashukuru watanzania kwa michango yao waliyoitoa kuisapoti Stars katika michezo ya kuwania kufuzu kwa Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi dhidi ya Algeria.

Farough aliwashukuru watanzania kwa kujitokeza kwa wingi katika mechi ya Taifa Stars na Algeria na wale wote waliosafiri na timu hiyo ya Taifa kwenda Algeria katika mechi ya marudiano.Mwenyekiti huyo amechukua fursa hiyo kuishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu, Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete,  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani na viongozi wote wa chama na serikali kwa njia moja au nyingine katika kuisapoti timu Taifa Stars kwenye mchezo na Algeria

Naye Mkuu wa mkoa Dar es Salaam, ambaye ni mlezi wa kamati hiyo,  Mecky Sadick aliwashukuru watu wote, kuanzia wanakamati kwa jinsi walivyojitoa kwa muda wao wote katika maandalizi na hasa kuhamasisha watanzania kujitokeza kwa wingi uwanjani kuishangilia timu yao ya taifa kwa kuonyesha uzalendo.

Katika mchakato mzima wa awali wa mechi ya kufuzu kombe la dunia 2018, Kamati kupitia kwa wadau mbalimbali iliweza kuchangisha Jumla ya Sh  122,640,000, dola 19,800 na Sh 177,000 kutoka tigo pesa na airtel money ambapo matumizi ni dola 70355, na Sh 47,904, 743 milioni

Post a Comment

 
Top