BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
MSHAMBULIAJI wa Azam FC  na timu ya Taifa ya Burundi, Didier Kavumbagu, amesema ushindi wa bao 1-0 walioupata jana katika mechi ya ufunguzi ya michuano ya Kombe la Chalenji dhidi ya Zanzibar ni mwanzo mzuri kwao.

Akizungumza na BOIPLUS, Kavumbagu alisema kuwa anafurahi kuona anatoa mchango kwa timu yake hiyo nafasi ambayo alikuwa akiililia kila siku wakati huo hapati nafasi ya kucheza Azam FC."Bado ligi ya sasa haijakaa vizuri kwangu kwani sipati nafasi ya kucheza mara kwa mara ingawa naona kwenye timu yangu ya Taifa wananitumia vizuri.

"Mara nyingi nimekuwa nikizungumza kuwa nahitaji nafasi ya kucheza maana najiamini kuwa naweza na uwezo wamgu ni mkubwa hivyo naamini ushindi huu ni mwanzo mzuri kwetu,'' alisema Kavumbagu

Burundi ipo Kundi B itashuka itacheza mechi yake ya pili Jumatano dhidi ya  Kenya, mechi itakayochezwa katika Mji wa Awassa.

Post a Comment

 
Top